Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad Al-Tayyib ametumia lugha ya Kifarsi katika ujumbe wake ili kulaani wazi uvamizi unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, na kutoa onyo kali kuhusu njama ya utawala huo ya kusababisha machafuko katika eneo la Mashariki ya Kati na kuligeuza kuwa uwanja wa mapigano na vita vya kudumu.
Sheikh wa Al-Azhar alisisitiza kuwa mashambulizi haya ya kimfumo na ukatili ya mara kwa mara yanaofanywa na utawala huo dhalimu na wa haramu, yanalenga kuliweka eneo hili kwenye ukingo wa mlipuko mkubwa wa vita, vita ambavyo watakao nufaika navyo ni wafanyabiashara wa silaha na damu tu.
Katika ujumbe wake wa Kifarsi kwenye Twitter, Sheikh Ahmad Al-Tayyib aliandika:
“Ninalaani vikali uvamizi wa mara kwa mara wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na mashambulizi ya kimfumo na ukatili endelevu wa utawala huu haramu na dhalimu, ambayo yote yanalenga kulifikisha eneo hili kwenye ukingo wa mlipuko mkubwa na kuanzisha vita vya jumla ambavyo ni wafanyabiashara wa damu na silaha pekee watakaonufaika navyo.”
Maoni yako